ALIYEWAHI kuwa kocha mkuu wa klabu ya Simba, Sven
Vandenbroeck amewapa mchongo waajiri wake hao wa zamani kwa kusema kama
wanataka kufanya vizuri kimataifa, basi ni lazima wahakikishe wanakuwa na
mshikamano na kutumia vizuri faida uwanja wa nyumbani kwani kundi walilopangwa
ni gumu.
Sven aliyeiongoza Simba kwa misimu miwili akihudumu kwa nusu
msimu kwenye kila msimu, alitangaza kuachana na Simba Alhamisi ya Januari 7,
mwaka huu muda mfupi baada ya kuipeleka Simba hatua ya makundi kwa kwa
kuiondosha FC Platinum ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 4-1.
Kocha huyo ambaye tayari amesaini mkataba wa miaka miwili
ndani ya kikosi cha Far Rabat ya Morocco aliipa Simba mataji matatu ambayo ni;
kombe la Ligi Kuu Bara 2019/20, kombe la FA 2019/20 na ngao ya jamii 2020/21.
Akizungumzia kundi ambalo wamepangwa waajiri wake hao wa zamani, Sven amesema Simba wamepangwa kundi gumu kutokana na ubora wa timu zilizopangwa kwenye kundi
hilo, lakini anaamini bado wana nafasi kubwa ya kufuzu hatua ya robo fainali.
“Ukiliangalia vizuri kundi ambalo Simba wamepangwa utagundua
wazi kwamba wana kazi kubwa ya kufanya kutokana na ubora wa timu walizopangwa
nazo, Al Ahly na AS Vita ni timu kubwa ambazo tayari zimefanya uwekezaji wa
kutosha kwenye soka hivyo siyo rahisi kuwashinda licha ya kuwepo kwa kumbukumbu
ya kufanya hivyo.
“Hata Al Merrikh sio wa kuwabeza, lakini naamini Simba bado
wana nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali kama watakuwa na umoja na kutumia
vizuri faida ya kucheza kwenye uwanja wao wa nyumbani, ni muhimu wakahakikisha
pointi tisa za nyumbani zinasalia kwao kabla ya kufikiria ni jinsi gani waapata
matokeo ya ugenini,” amesema Sven.
Akiwa na kikosi cha Simba Sven aliingoza timu hiyo kwenye
michezo 55 akishinda mechi 39, amepoteza mechi sita na kutoa sare michezo kumi
Kwa ushauri huo kwa Nini umewakimbia?
ReplyDeleteKwa ushauri huo kwa Nini umewakimbia?
ReplyDeleteWataongea mengi, watatokea washauri na walimu wengi tu mwishowe kelele. Simba niteam inayojiekewa
ReplyDeleteKuna kipi kipya hapo ambacho Simba hawakijui, huo mchongo umejipa wewe mwenyewe kanjanja
ReplyDelete