January 28, 2021

 


MSHAMBULIAJI mpya wa kimataifa wa Yanga raia wa Burundi, Fiston Abdoul Razak anayecheza kama pacha wa Said Ntibazonkiza 'Saido' kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi, tayari ameanza safari ya kuja Tanzania kwa ajili ya kujiunga na kambi ya kikosi hicho inayojiandaa na michezo ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Mshambuliaji huyo ni miongoni mwa nyota watatu waliokamilisha usajili wa kujiunga na kikosi cha Yanga katika dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15.

Nyota huyo anatajwa kuwa hatari hasa anapocheza na pacha wake Saido ambapo akiwa na kikosi cha Burundi katika michezo ya kufuzu michuano ya AFCON amefanikiwa kuweka kambani mabao sita, hivyo kuongoza chati ya wafungaji pamoja na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Nigeria na Klabu ya Manchester United Odion Ighalo.

Akizungumzia kuhusu ujio wa nyota huyo kabla ya kusimamishwa majukumu yake, Ofisa habari wa Klabu ya Yanga Hassani Bumbuli amethibitisha kuwa nyota huyo yupo njiani kuja kujiunga na wenzake na kuwaomba Wanayanga wajitokeze kwa wingi kama ilivyo kawaida yao

“Mshambuliaji wetu, Fiston Abdoul Razak anatarajiwa kuwasili nchini hivi karibuni akitokea kwao Burundi kwa ajili ya kujiunga na kambi ya Yanga inayoendelea kujiandaa na michezo ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara chini ya kocha Cedric Kaze.

“Kama kawaida yetu Wanayanga tunaomba mjitokeze kwa wingi kwa ajili ya mapokezi hayo,” alisema Bumbuli.

4 COMMENTS:

  1. Ikiwa mwenye kiwango cha Morrisson na kwakuwa mkataba wake ni wa miezi sita tu, basi mkizubaa kidogo upepo utampeleka Msimbazib

    ReplyDelete
  2. Endea hivyo hivyo kuwa na mawazo ya kizamani boy

    ReplyDelete
  3. Tuliambiwa anafika leo, imekuwaje tena, au anakuja kwa bus la Saratoga au Adventure?

    ReplyDelete
  4. Uongozi tupeni ratiba kamili tukampokee airport

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic