NYOTA mpya wa Klabu ya Yanga, Razack Adulazack amesema kuwa amesaini mkataba wa miezi sita hivyo atapambana kufanya vizuri katika muda huo ili aweze kutimiza majukumu yake.
Razack anakuja ndani ya Yanga inayonolewa na Cedric Kaze kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo inaongozwa na Michael Sarpong na Yacouba Songne ambao wametupia mabao mannemanne.
Nyota huyo amesema:"Nimesaini mkataba wa miezi sita kwa ajili ya kutimiza majukumu yangu ndani ya Yanga, imani yangu ni kwamba kwa muda ambao nitakuwa kikosini nitafanya juhudi kutimiza majukumu yangu kwa wakati.
"Kikubwa ni ushirikiano nina amini kwamba kila kitu kitakwenda sawa naomba mashabiki wawe pamoja nami," .
Raia huyo wa Burundi anaungana na mshikaji wake Saido Ntibanzokiza ambaye yupo ndani ya kikosi hicho ambacho kimetwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.
festo; mkataba wa miezi 6 afu badae mseme miaka miwili
ReplyDeleteHayakuhusu
DeleteSi wameshakuambia ni miezi 6 sisi akituzingua tutamuonesha clip za Morrison na kwa sasa anafanya nn
DeleteUTO wazee wa miba
Delete