January 31, 2021


 MWISHO wa ubishi ni leo kwa mchezo wa kirafiki kati ya Global FC dhidi ya timu ya DStv mchezo unaotarajiwa kupigwa kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Mchezo huo ambao ni maalum kwa ajili ya kudumisha uhusiano na ujamaa kati ya Kampuni ya Multichoice na Global Group ambazo zimekuwa zikishirikiana kwenye mambo mbalimbali unatarajiwa kuwa na upinzani wa aina yake kutokana na maandalizi ya timu zote mbili.

 

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Global FC, Philip Nkini amesema kuwa kikosi chake kimekamilika na wanaamini wataibuka na ushindi ndani ya dakika 90.

 

“ DStv waje kwa nidhamu tumefanya maandalizi kwa muda mrefu na itakuwa ni mechi yetu ya kwanza kwa ufunguzi ndani ya 2021 hivyo tutafanya jambo la kweli, mashabiki wajitokeze kwa wingi.

 Nahodha wa DStv, Festo Laizer amesema: “Mpira hauchezwi mdomoni ni ndani ya uwanja,tutafanya kweli na hakuna ambacho kinashindikana tutawafunga na hawataamini,”.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic