January 31, 2021


MARCUS Rashford, mshambuliaji wa Klabu ya Manchester United amesema kuwa anatambua kwamba ana rangi nyeusi anaifurahia rangi hiyo wale wanaombagua hawatendi jambo la haki na wala wasifikiri kwamba atawajibu.

Nyota huyo wa Manchester United alikutana na jambo hilo kupitia mitandao ya kijamii muda mfupi baada ya timu yake kulazimisha sare ya bila kufungana dhidi ya Klabu ya Arsenal, Uwanja wa Emirates kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram mashabiki walianza kumshambulia Rashford kwa kutumia emoji za nyani na wengine waliweka ujumbe kwamba anapaswa kwenda maeneo ya makazi ya wanyama jambo ambalo limemuumiza nyota huyo kuhusu ubaguzi wa rangi.

Mbali na Rashford mwenye miaka 23 pia suala hilo la ubaguzi wa rangi lilimtokea nyota mwenzake Axel Tuanzebe na Anthony Martial pia nyota wa Chelsea Reece James na nyota wa Klabu ya West Broms Romaine Sawyer nao pia walikutana na ubaguzi kwenye mitandao ya kijamii.

Rashford kupitia tweet amesema:"Utu na mitandao ya kijamii umekuwa kwenye wakati mbaya kwa sasa. Ndio ninajua kwamba mimi ni mweusi na ninaishi na katika hilo ninajivunia kabisa kwa rangi ambayo ninayo. 

"Hapana, hapana, ujumbe wowote ambao utauandika hapa ama hakuna mtu yoyote yule ambaye anaweza kunifanya nijiskie tofauti.

"Samahani ikiwa unahitaji kuona ninaweza kuchukulia tofauti hilo haliwezi kutokea kwangukiwepesi tu hautaona kwangu samahani. Kuna watoto wazuri ambao wanaipenda rangi yangu na wanafuata ndoto zao siwezi kuwaangusha," .




1 COMMENTS:

  1. Watu hawana akili, kama wao wanaweza ni kwa nini hawamo kwenye timu ya Man U? Mpira unataratibu zake na ufundi na ugumu wake pia, sio sawa na kushabikia tuu wakati huwezi hata kufunga goli lisilo ja golikipa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic