January 28, 2021


 THOMAS Ulimwengu nyota Mtanzania anayekipiga ndani ya kikosi cha TP Mazembe amesema kuwa anafurahi kurejea nyumbani akiwa na timu yake hiyo ya Congo.

Ulimwengu amekuwa akitimiza majukumu yake vizuri ndani ya timu hiyo jambo ambalo limekuwa likimfanya awe na furaha kwenye maisha yake mapya na timu hiyo kubwa barani Afrika.

Ni miongoni mwa washambuliaji ambao walifanya kazi kubwa ya kufunga wakati timu hiyo ikitinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

TP Mazembe ni miongoni mwa timu shiriki kwenye Simba Super Cup ambapo wao ni wageni wakiwa wamealikwa na waandaaji wa mashindano hayo ambao ni Simba.

Jana Januari 27 wakati Simba ikifanya ufunguzi na kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 Uwanja wa Mkapa alikuwa miongoni mwa wachezaji wa TP Mazembe ambao walishuhudia mchezo huo.

Timu yake kesho Januari 29 itamenyana na Al Hilal na itakutana na Simba Jumapili na Simba , Uwanja wa Mkapa.

Mshambuliaji huyo amesema:"Ninaipenda nchi yangu Tanzania na ninafurahi kuwa tena ndani ya Tanzania pamoja na timu yangu ambayo nipo kwa sasa," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic