Samatta alifunga bao hilo
dakika ya 51 ya mchezo huo wa Turkish Cup raundi ya 16 uliopigwa kwenye Uwanja wa Şükrü
Saracoğlu, ambapo alianza kwenye kikosi cha kwanza kabla ya kutolewa dakika ya
69 na nafasi yake kuchukuliwa na Ozan Tufan.
Samatta amekuwa nje ya Uwanja tangu
mwezi Novemba mwaka jana kutokana na majeraha ya misuli ambayo yalimfanya akose
michezo ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya AFCON ambapo Taifa Stars ilipepetana dhidi ya Tunisia Novemba 13, na 17.
0 COMMENTS:
Post a Comment