UONGOZI wa Simba umesema kuwa bado haujapata vibali vya kumtumia mchezaji wao mpya, Perfect Chikwende,(ITC) kutoka Shirikisho la Soka la Zimbabwe ila wanaamini watavipata hivi karibuni.
Nyota huyo anaingia kwenye kumbukukumbu za kuwa nyota ambaye alimtungua Aishi Manula ugenini kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwa mchezo wa kwanza wa Simba dhidi ya Plateau United Manula hakufungwa ugenini msimu wa 2020/21.
Kwenye mchezo huo uliompa ulaji uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe Chikendwe alitumia makosa ya mabeki kusepa na mpira na kumtungua Manula wakati FC Platinum ikishinda kwa bao 1-0.
Amesaini dili la miaka miwili kutumika ndani ya Klabu ya Simba ambayo kwa sasa inanolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes aliyetwaa mikoba ya Sven Vandenbroec ambaye yupo zake FAR Rabat ya Morocco.
Mtendaji Mkuu wa Simba, (CEO), Barbara Gonzalez amesema kuwa bado hawajapata ITC ya Chikwende kutokana na kile anachodhani kuwa ni utaratibu wa mtandao wa Zimbabwe.
"Shirikisho la Zimbabwe limekuwa taratibu sana kwenye upande wa kuthibitisha na kujibu kuhusu haya ila nina amini kwamba kati ya siku hizi mbili ama tatu inaweza kuwasili.
"Bado tunaisubiri ITC kwetu sisi tumekamilisha kila kitu kwa upande wetu hasa kwenye mtandao hilo unaweza kuona kwamba kwa mchezaji wetu Lokosa,(Junior) kutoka Nigeria tayari ITC yake tumepata," .
Lokosa mabaye ni mshambuliaji jana alikuwa benchi wakati timu yake ikishinda mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal ya Sudan huku Chikwende akiwa ni miongoni mwa wale ambao walianza.
Katika mabao hayo manne aliweza kufunga bao moja baada ya kipa wa Al Hilal kutema shuti lililopigwa na Bernard Morisson.
Huyo anshitajika kwa kuwafumba midomo wale wanaojidanganys eti ubingwa ni wao
ReplyDelete