February 10, 2021


KESHO kikosi cha Azam FC  kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kitakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Coastal Union. 


Msafara wa kikosi hicho chenye wachezaji 23 umewasili Tanga usiku wa jana Februari 9 ukiwa na Ayoub Lyanga mwenye jumla ya mabao matano ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kuwatungua Simba kwenye sare ya kufungana mabao 2-2, Uwanja wa Mkapa.

Lyanga ni zao la Coastal Union hivhivyoeo anakwenda kukutana na mabosi zake wa zamani kabla ya kesho kukutana nao ndani ya Uwanja wa Mkwakwani.


Mchezo wao wa mzunguko wa Kwanza, zama za Arstica Cioaba Azam FC ilishinda mabao 2-0, Uwanja wa Azam Complex.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic