KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes leo Februari 10 kinatarajiwa kuendelea na safari kuelekea Congo kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao ni wa hatua ya makundi.
Jana, Februari 9 msafara wa wachezaji pamoja na benchi la ufundi waliweka kambi kwa muda Addis Ababa baada ya kuwasili hapo wakitokea Bongo, hivyo leo watamalizia ngwe ya safari ya mwisho.
Katika msafara huo ni nyota wawili ambao wamebaki Bongo ambao ni Perfect Chikwende yeye ni maalumu kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na nahodha John Bocco ambaye anasumbuliwa na majeraha aliyopata kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.
Hivyo nyota hao wawili wataukosa mchezo huo. Huku nyota Jonas Mkude ambaye alikuwa nje akitumikia adhabu ya utovu wa nidhamu yupo ndani ya kikosi.
Simba itatupa kete yake ya kwanza Februari 12 dhidi ya AS Vita ya Congo inayonolewa na Florent Ibenge ambaye anazijua mbinu za Simba.
Waliwahi kukutana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi msimu wa 2018, Simba ililala mabao 5-0 na kipa alikuwa ni Aishi Manula, zama za Patrick Aussems ambaye yupo zake ndani ya AFC Leopards ya Kenya.
Gomes amesema:"Tunatambua utakuwa mchezo mgumu ila kazi yetu ni kupambana kusaka ushindi ndani ya uwanja na inawezekana,".
Kwahiyo plan ya kumleta Chikwende kwa ajili ya mechi za kimataifa imefeli!!!!!!
ReplyDeleteChikwende anaweza kucheza hatua zinazofuata lakini si hii ya makundi kwa vile alishaichezea Platinum FC
DeleteSimba walimuhonga morison yanga ikapigwa 4, simba walimuhonga chikwende platinum ikapigwa 4, saiz naona wataenda kwa shishimbi...
DeleteVidimbwi FC wanajitahidi kuichafua Simba lakini watu hawawaelewi,ndo Kwanza kocha anaacha kazi El merreikh anakimbilia Simba teh teh teh teh teh watabakia na propaganda Simba inazidi kupaa,huyo Morrison na Chikwende wanacheza peke yao uwanjani
DeleteDuh! Akili zako ndio zimeishia hapo? Hakika kidimbwi ni kidimbwi tu.
Delete