February 24, 2021


 WAKATI mwingine unaweza kupata kila kitu kwenye maisha yako ila ukakosa matumaini hapo matatizo yanaanza hasa kwa mmiliki wa kile ambacho anacho na yule ambaye anahitaji kumiliki.

Hasa pale mitaa ya Kariakoo kumekuwa na mambo ambayo yanatokea na ukisikiliza kila mmoja anavutia kamba upande wake ili kuonekana yupo sawa na kusahau kwamba mpira ni dakika 90.

Unamkumbuka yule mwamuzi ambaye alichezesha mchezo wa Tanzania Prisons 1-0 Simba, alifungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kwa kosa la kushindwa kuumudu mchezo ule.

Mchezaji ambaye analeta mgogoro kwenye ligi, Bernard Morrison ambaye yupo zake Simba kwa sasa alionekana akichezewa faulo ndani ya 18, mwamuzi akapeta na maisha yakaendelea kama kawaida.

Unamkumbuka yule mwamuzi wa KMC 1-2 Yanga, ile penalti matata iliyotolewa kwa Yanga baada ya Michael Sarpong kuangushwa ndani ya 18 maisha yake yapoje na namna gani alilamikiwa na wapinzani.

Weka kando kwamba kuna mechi ya Mbeya City 1-1 Yanga, bao lilionekana na utata na kuna penalti ya Yanga ilipaswa kutolewa ila ikapetwa na Mbeya City walipata penalti wakafunga.

Bado maisha yanaendelea rudi nyuma pale Gwambina Complex, Gwambina 0-0 Yanga, Gwambina walifunga bao likafutwa kwa kile kilichoelezwa kuwa kuna mchezaji wa Gwambina alikuwa ameotea.

Kabla ya bao hilo kufungwa inaonekana dhahiri kona waliyopata Gwambina ilikuwa na utata mwisho wa siku bao lake nalo likaleta utata.

Haya maisha ya Kariakoo ni magumu kwa kweli sijajua tatizo lipo wapi. Labda ningependa kuwashauri Simba wamrudishe Morrison kwa Yanga iwe kwa mkopo ama kwa kupenda ili kupunguza hizi filamu za kila siku.

Ndio labda tatizo ni Morrison kwa sababu kila atakavoboronga ama kufanya vizuri utaskia watu wanazungumza na kuanza kutoa yale ya moyoni.

Huyu Morrison ni tatizo kubwa kwenye soka letu na sio kitu kingine mimi ninadhani ipo hivyo ama wewe unadhani kuna tatizo gani. Nadhani unakumbuka kuna mchezo pale Uwanja wa Mkapa alitoa pasi kwa mgongo unajua siku ya pili nini kilitokea, sijui nikumbushe.

Ila kwa nini Simba hawaonekani kulalamika kuhusu waamuzi wao wanaendelea na maisha yao kama kawaida ndani ya uwanja na nje ya uwanja wanajua wao.

Hapo kuna kitu cha kujifunza na kuona namna gani maisha yanaweza kuendelea bila uwepo wa malalamiko katika kutafuta haki.

Yanga waliweka wazi kwamba huenda wangejitoa kushiriki ligi ikiwa mwamuzi wa mchezo wa Februari 20 kati yao dhidi ya Yanga asingetenda haki. Huku ni mbali sana tunafika.

Bado sijui haya mawazo yapoje labda tusubiri na tuone ila mchezo ndani ya uwanja unahitaji maandalizi na kila mmoja ni lazima atambue kwamba mwamuzi naye ni binadamu makosa yapo hata Ulaya ndio maana wanatumia VAR ila simaanishi wasifanye vizuri.

Bado soka letu ni pasua kichwa, waamuzi pasua kichwa ,viongozi wengine pia ni pasua kichwa kuna kazi kubwa kuyafikia mafanikio.

Makala haya iliandikwa ndani ya Gazeti la Championi na Oscar Oscar.

 

10 COMMENTS:

  1. hueleweki unaonekana umevurugwa.Simba baba lao

    ReplyDelete
  2. Oscar umezunguka sana. Waambie tu yanga waache mdomo mpira hawaujui

    ReplyDelete
  3. Yanga wanalalamika kila wakitoa sare. 😃 Mbona simba tunanyimwaga penalt na michezo huohuo tunafungwa lakini hatulalamiki?

    ReplyDelete
  4. Tff ya Simba mnaongoza kwa kubebwa marefa wanachezesha kwa maagizo ya tff mtalalamika nini acheni tulalamike cc ambao tunaonewa osca mwenyewe kiherehere wa Simba anashauri nini mnafiki shoga tu hyo.

    ReplyDelete
  5. Ivi tukikuukiza ulichokiandika unaweza kutuambia?,maana hakuna maana yoyote iloyotengenezwa hapo

    ReplyDelete
  6. Nimerudia kusoma mara mbili lakini sijaelewa ujumbe unaotaka kutuletea.

    ReplyDelete
  7. hakuna ujumbe hapo na wew ni walewle badala ya kusema ukweli unaanza kutetea nn sas,,,hapo hujatoa ujumbe wowote bali kuna sehemu unatetea,,,tafakari usituambie tena mambo yako sis haytuhusu,,na Kwa waamuzi kama hao czani kama czan kama soka la tz litaendelea,, kama kila kukicha tunaendelea kuteea maovu,,

    ReplyDelete
  8. Sijakuelewa ulitaka kuzungumza nn kijana,ila tatizo linaazia kwenu unazi ukizidi upande mmoja

    ReplyDelete
  9. Bernard Morrison ana umuhimu mkubwa sana ndani ya timu ya Simba kwa sasa. Tuangalie umuhimu katika mechi zote zinazokuwa ngumu kwa Simba yeye analeta matokeo chanya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic