February 5, 2021


DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mchezo wake wa jana Februari 4 dhidi ya Dodoma Jiji ulikuwa mgumu ila wamefanikiwa lengo lao la kutwaa pointi tatu.

Timu ya Simba ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Gomes ndani ya ligi baada ya kupewa mikoba ya Sven Vandenroeck.

Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere na lile la ushindi lilifungwa na Bernard Morrison huku lile la Dodoma Jiji likifungwa na Cleophance Mkandala.

Gomes amesema:-"Tulitambua kwamba utakuwa mchezo mgumu tangu awali kwa kuwa ligi ipo tofauti na ni ngumu, kila timu inahitaji pointi tatu hivyo nimeona wachezaji wangu walipambana.

"Kwa ushindi wa mwanzo sasa hapo tunageuza nguvu zetu kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya Azam FC kwani lengo la kwanza ni pointi tatu kisha mambo mengine yanafuata.

"Hii itatusaidia kupunguza pointi ambazo tumeachwa na yule anayeongoza ligi hivyo bado tuna kazi kubwa ya kufanya," .

Simba inafikisha pointi 38 ikiwa imecheza mechi 16 imeachwa kwa jumla ya pointi sita na vinara Yanga ambao wana pointi 44 wakiwa wamecheza jumla ya mechi 18.

Mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Azam FC utakaochezwa Februari 7, Uwanja wa Mkapa na leo kikosi kitarejea Dar kutoka Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic