February 5, 2021


 MABINGWA wa kihistoria Tanzania, Yanga wamesema kuwa wapo tayari kumlipa mchezaji wao wa zamani Amiss Tambwe ambaye anawadai fedha za usajili pamoja na mshahara wakati akitumika ndani ya kikosi hicho.

 

Tambwe alikuwa ni mshambuliaji na pia aliwahi kucheza kwa watani zao wa jadi Simba kabla ya kuachwa na kuibukia ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

 

FIFA ilitangaza kuifungia Yanga kwa kile kilichotajwa kutomlipa mshambuliaji huyo madai yake ya Sh milioni 44 yaliyotokana na usajili wake.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alisema kuwa mashabiki wasiwe na hofu juu ya hukumu hiyo ya FIFA, wamejipanga vema kufanikisha hilo na wataendelea kufanya usajili kama kawaida.

 


“Mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi kabisa hizo milioni 44 tutazilipa haraka iwezekanavyo, tulivyoingia madarakani tulikuta madeni mengi katika timu, hivi sasa tumeyalipa na tunaendelea kuyalipa,” alisema Mwakalebela.

 

Alipotafutwa Tambwe kuzungumzia hilo, alisema: “Hiyo adhabu waliyoitoa FIFA ni kweli, lakini kama watalizilipa hizo fedha wataruhusiwa kuendelea na usajili kama kawaida, ".



13 COMMENTS:

  1. Kwa hiyo kuweka sawa kumbukumbu, ni kwamba hadi sasa Yanga wameshafungiwa kusajili kwa miaka mitatu mfululizo. Suala la kuja kumlipa ili wafunguliwe hilo ni lingine kabisa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hayo ni maoni yako Tena wangetufumgia miaka 5 maana sisi wachezaji tulionao ni watoto wadogo Wana miaka sits mbele

      Delete
  2. Eti kila Morison anapofunga goli, kesho yake Mwakalebela anaitisha press kuelezea maendeleo ya kesi huko CAS =))

    ReplyDelete
  3. Kwanini tusiwe na wasiwasi nayni wazito kuwalipa wachezaji haki zao, ikiwa leo ni Tambwe labda kesho itakuwa Saido na hapo tena nini itakuwa morali ya wachezaji wanaoteseka kwaajili timu ambao watahisi hawana dhamana ya ya maisha yao ya kimchezo nao pia watazurika

    ReplyDelete
    Replies
    1. Imedaiwa serikali sembuse Yanga,imedaiwa Madrid sembuse Yanga we vp

      Delete
  4. Mnalipa baada ya kuamriwa na FIFA...kwa kulàzimishwa!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kumbuka sir tunadaiwa mil 44, Simba imepelekwa mahakamani na meneja wenu Patrick mnadaiwa mil 80.malizeni la kwenu kwanza

      Delete
    2. We unatakaje ,achana na yanga yet bhn,na mwaka huu mtaendelea kuangalia tu makombe yanavyo bebwa .yana simba wamekosa yakuongea ndan ya Moira wanafwatilia mambo yalio nje,kumbuka hujanifunga mbaka sasa katika mech mbil tulizo kutana

      Delete
  5. Kenge mpaka atolewe damu ndio anajitambua.Akitoka damu puani anajua kaumia. Utopolo bila mikwaju hawatembei.Eymael alisema kwelim

    ReplyDelete
  6. Simba manakomaa na Yanga, hamjui kuwa na nyie mnadaiwa na Patrick Mwijage mil 80? Tena kesi iko mahakamani

    ReplyDelete
  7. Akishinda atakuwa na haki ya kulipwa.

    ReplyDelete
  8. Mlipeni tambwe pesa zake,na wale wengine wanawadai bado hamjawalipa kazi midomo tu, mnazindua siku ya kalenda, siku ya vyombo vya habari n.k wanawaza upumbavu tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic