February 5, 2021

 


LICHA ya kikosi cha Tottenham kupoteza mchezo wake wa Ligi Kuu England kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Chelsea, Jose Mourinho, Kocha Mkuu wa timu hiyo amesema kuwa anaona moyo wa upambanaji kwa wachezaji wake.

Tangu iliposafiri kuibukia ndani ya Anfield, Desemba 16 Tottenham imepoteza jumla ya mechi tano kati ya tisa ambazo imecheza na mitatu kati ya hiyo imekuwa ni mfululizo tangu kuanza kwa 2021.

Matokeo hayo kwenye mechi za Ligi Kuu England ilikuwa Tottenham 1-3 Liverpool, Brighton 1-0 Tottenham na Tottenham 0-1 Chelsea na bao la ushindi lilifungwa na Jorginho kwa mkwaju wa penalti.

Matokeo hayo yanaifanya Chelsea kufikisha jumla ya pointi 36 ikiwa nafasi ya 6 baada ya kucheza jumla ya mechi 22 na Tottenham inabaki na pointi 33 ikiwa nafasi ya 8 baada ya kucheza mechi 21.

Mourinho amesema:"Bado ninaona moyo wa upambanaji kwa wachezaji wangu wakiwa uwanjani, tupo pamoja na tunafanya kazi kwa pamoja hilo ni jambo jema kwangu na timu.

"Kingine ni hali ya kujiamini pia ipo, unajua ikiwa unashindwa kupata matokeo na timu yako inacheza vizuri kuna mabo ambayo ni lazima yafikiriwe ndani ya timu, ila sio mbaya kwa hapa ambapo tupo," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic