NYOTA watatu wa Azam FC wanatarajiwa kuukosa mchezo wa kesho dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili ambazo zipo ndani ya tatu bora.
Simba ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza jumla ya mechi 16 na ina pointi 38, Azam FC ipo nafasi ya tatu ina pointi 32.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam, Zakaria Thabit amesema kuwa nyota hao ni beki Yakub Mohamed ambaye ana kadi tatu za njano.
Kiungo Frank Domayo ambaye anasumbuliwa na majeraha ya goti atakuwa nje mwezi mzima.
Na beki Abdul Omary Hamahama.
Tuta wapga hvohvo
ReplyDeleteSimba A vs Simba B. Hakuna mechi hapo
ReplyDeleteKama kawaida yenu, mnaanza mapemaaa simba akishinda tayari mnazo sababu zenu mlizokwisha ziandaa, dah kuna watu mmeumbwa na akili fupi sana ila mungu awasaidie, sijui ni lini mtaishiwa sababu,mbona ninyi mlicheza na mkawafunga au ni ninyi ni AZAM B?mfa maji haachi kutapatapa, kazaneni mtafanikiwa.
Delete