February 8, 2021


 TUISILA Kisinda, nyota wa kikosi cha Yanga amesema kuwa hana mpango wa kucheza ndani ya Simba kwa kuwa maisha yake kwa sasa yanaendelea vizuri ndani ya mtaa wa Jangwani.

Nyota huyo ambaye ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze ni miongoni mwa viungo ambao wanafanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kulikuwa na habari kwamba miongoni mwa nyota ambao wanahitajika ndani ya Simba ni pamoja na Kisinda jambo ambalo nyota huyo ameligomea.

"Kwa sasa bado nipo ndani ya Yanga na sina mpango wa kuondoka hivyo mashabiki wasiwe na mashaka sifikirii kwenda Simba.

"Maisha yetu ndani ya kikosi ni mazuri na kila mmoja anafurahi kile ambacho anakifanya hivyo ni wakati wetu wa kuendelea kufanya vizuri," .

Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa imekusanya jumla ya pointi 44,imecheza mechi 18 bila kupoteza huku ikiwa imeshinda mechi 13 na ina sare 5.

4 COMMENTS:

  1. Simba hawawez kuhitaji mchezaji wa aina hiyo anayekimbia bila mipango,mbio nyingi halafu mwishoni kazi bure.

    ReplyDelete
  2. Labda alihitajiwa na simba ya congo

    ReplyDelete
  3. Aache ujinga huyo hana hadhi kwa simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ata Morrison mlisema ivyo ila baadae ilikuwaje

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic