CHRISTINA Mwagala, Ofisa Habari wa Klabu ya KMC amesema kuwa walitoa tahadhari mapema kwa wapinzani wao Namungo kabla ya kukutana nao uwanjani kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara.
Timu ya KMC ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Namungo, Uwanja wa Uhuru na kusepa na pointi tatu muhimu.
Mabao ya KMC yalifungwa na Matteo Anthony dakika ya 8, Charles Ilanfya dakika ya 58 na Rodgers alijifunga dakika ya 90+2.
Christina amesema:-"Tulisema kwamba Namungo hatuibezi ila tumeitembezea pira kodi,pira mapato na pira spana halafu tukapata pointi tatu.
"Pongezi kwa wachezaji pamoja na mashabiki ambao wanaipa sapoti timu yao bado kazi ni kubwa na tumemaliza mchezo wetu wa kiporo kazi inayofuata ni kwenye mechi zetu za mzunguko wa pili," .
Kwenye msimamo wa ligi, KMC ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza jumla ya mechi 18.
Namungo FC imekuwa na mwendo wa kusuasua msimu wa 2020/21 ipo nafasi ya 15 baada ya kucheza jumla ya mechi 15 ikiwa na pointi 18.
Namungo wanasubiri kukaza kiporo Cha Simba , ambacho Simba wamesema Kula kiporo Cha korosho Ni RAHISI sawa na kumsukuma mlevi
ReplyDelete