CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa jambo litakalomuongezea kasi mshambuliaji wake Michael Sarpong pamoja na Yacouba Songne kutupia mabao mengi ni kupokea mipira kutoka pembeni na kati kutoka kwa viungo wake.
Sarpong
na Yacouba ambao ni washambuliaji kwa pamoja wamehusika kwenye jumla ya mabao
12 kati ya 29 yaliyofungwa na timu hiyo inayoongoza ligi ikiwa na pointi 44
baada ya kucheza mechi 18.
Sarpong
ametupia mabao manne sawa na Yacouba ambaye ana pasi nne za mabao wote ikiwa ni
msimu wao wa kwanza kuwa ndani ya kikosi cha Yanga.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Kaze amesema kuwa kazi ambayo amewapa viungo wake wa pembeni
ambao ni Farid Mussa na Carlos Carlinhos ni kutoa mipira kwa kuugawa uwanja.
“Sasa
nimegundua tatizo ni kwamba washambuliaji wanakosa mipira ya kuijaza nyavuni
kwa kuwa inatoka upande mmoja, nimewaambia viungo wangu kuwa waugawe uwanja kwa
kutoka pembeni na kati pia.
“Ikiwa
watatoa pasi kutoka pembeni na wengine watatoa pasi kutoka katikati itaongeza
hali ya washambuliaji kuwa kwenye nafasi nyingi uwanjani na kufunga namna
ambavyo wanataka na inawezekana,” amesema.
Kesho, Februari
13, Yanga itamenyana na Mbeya City, Uwanja wa Sokoine ikiwa na kumbukumbu ya
kushinda kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Hahahaa, ngoja tuone hiyo kesho
ReplyDelete