February 5, 2021


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa ulikuwa kwenye mpango wa kuinasa saini ya kiungo chaguo la kwanza la Didier Gomes ndani ya kikosi cha Simba, Rarry Bwalya ila dili hilo lilibuma kutokana na kuhofia kupigwa mkwanja mrefu.

Bwalya akiwa na Simba chini ya Kocha Mkuu, Gomes ambaye ni mrithi wa mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye alibwaga manyanga ndani ya Simba, Januari 7 ameanza kikosi cha kwanza kwenye mechi zote tatu.

Ilikuwa mbili za Simba Super Cup na moja ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji, kabla ya kuibukia Simba alikuwa anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga ameweka wazi kuwa walikuwa kwenye mazungumzo na nyota huyo ila wakamkosa kwa kuwa waliamua kuachana naye.

 “Wakati wa usajili tiulikuwa na hesabu za kumsajili pia Larry Bwalya kwa kuwa tulifanya nae mazungumzo kwenye hatua za mwanzo ila ofa kutoka klabuni kwao ilikuwa kubwa na tuliiona haiendani na bajeti yetu ya usajili.

“Wakati tunamtaka sisi alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja ambao tulitakiwa kuuvunja kwa kulipia vipengele vitatu ambavyo vilikuwa kwenye mkataba wake ambavyo ni fedha ya uhamisho ambayo ingeenda kwa klabu yake,fedha ya kusaini mchezaji ambayo ingeingia moja kwa moja kwa mchezaji na fedha ya wakala.

"Kutokana na mwendo huo kuwa mrefu tuliiona kwamba ni jambo ambalo huenda tungepigwa kwa kuwa ilikuwa ni fedha ndefu.

“Hatujutii kumkosa Bwalya kwa kuwa si mchezaji wetu na bado tunaongoza ligi,” amesema Hersi.

Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18, Simba yenye Bwalya ipo nafasi ya pili na pointi 38 baada ya kucheza jumla mechi 16.

8 COMMENTS:

  1. Lakini si walisema kwa bei yoyote wapo tayari kwa mchezaji ambae kikosi cha ufundi litamhitajia ni vipi leo wanalia mateka kwa kusema wameishindwa kwasabau mkwanja walioutaka ulikuwa mzito mno kuubeba

    ReplyDelete
  2. Si huwa mnadai kwamba hakuna mchezaji mnayemtaka mtashindwa kumchukua kwa kigezo cha gharama, mbona sasa unakiri kwamba bajeti haikutosha? Sasa wakati mwingine usiwafariji wana Yanga kwamba mnaweza kuvunja mkataba wa mchezaji wa timu nyingine mnayemtaka, Umekiri mwenyewe kwamba Larry Bwalya mlimtaka ila hela kwenu ikawa haitoshi

    ReplyDelete
  3. Kumchalenji Mnyama anayotafanya ni sawa na kupigwa vichwa vyenu juu ya ukuta. Wana wivu na mchumba wasueweza kumchumbia. Masikini roho zenu na Mnyama anakupigieni hodi

    ReplyDelete
  4. Hawa wanasubiri wachezaji huru kama fiston, yackoub , sarpong, seydou nq hata chama kelele zote walikuwa wanasubiri mlataba wake uishe

    ReplyDelete
  5. Jamani soka ndicyo ilivyo. Unasajili pale uwezo unaruhusu

    ReplyDelete
  6. Kwahivo mnakiri uwezo hamnao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic