UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema unajivunia mafanikio makubwa waliyoyapata msimu huu kwa kutwaa taji la kombe la Mapinduzi, pamoja na kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara mpaka sasa.
Yanga mpaka sasa ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo kwenye ligi, ambapo wamejikusanyia pointi 44 baada ya kucheza michezo 18, wakishinda mechi 13 na kutoa sare michezo mitano pekee.
Akizungumzia mipango na mafanikio yao msimu huu Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM na mjumbe wa kamati ya usajili ya Yanga, Injinia, Hersi Said amesema: “Tumefanya uwekezaji mkubwa ndani ya kikosi chetu msimu huu, na sisi sote tunakubaliana kwamba tayari matunda yameanza kuonekana kupitia ubingwa wa mapinduzi na mwenendo mzuri kwenye ligi.
“Tunashukuru Mungu katika hilo na
wakati huu tumebaki na lengo moja tu la kuhakikisha tunaibuka mabingwa msimu
huu.
Sawa kabisa
ReplyDeleteWords my brother!! Kuna timu hapa bila mchezaji flani kucheza hamna kitu milele
ReplyDeleteUna maana bila Chama?
DeleteUjinga wa kutambia Mapinduzi Cup. Azam kachukua mara 5 husikii wakisema ni mafanikio!!!
ReplyDeleteMapinduzi Cup imekuwa mafanikio???
Kuongoza ligi mmeongoza kwa miaka 3 lakini bingwa anajulikana.
ReplyDeleteMapinduzi na Simba super cup Nani zaidi?
ReplyDeleteMapinduzi "big up" sio la maigizo
DeleteSasa mbona yule Bonjour katamba nalo?,shida hapa ni uelewa na age .Hata Hiyo Mapinduzi ukiangalia Wananchi tulibaka walishandaa Bingwa wao ndiyo maana eti Opiyo Mchezaji Bora?,tukaharibu mpango hata Ile Hundi mfano ya Mchezaji Bora ukiangalia Tarakimu Ile ya mwanzo ni Kama iliandikwa palepale Uwanjani najua wengi hamkuiona.Inawezekana waliandaa laki tano wakijua Paka atakuwa Bingwa baada ya kukosa wakabadili figure ili wawaridhishe makauzu (Zingatia haikuwa na maneno Ila Tarakimu tu)
ReplyDeleteDaah kweli maisha yanakwenda kasi Sana leo hii yanga kuongoza ligi kwao ni mafanikio makubwa.... Kweli Mnyama amewapoteza vibaya
ReplyDeleteKombe la mapinduzi kwa njia ya bahatinasibu kwa panelti ndio mafanikio makubwa kwa matopolo ambayo wanayoyataja kila kukicha. Wanasema hiyo ndio fahari yao na jee pindi wakibahatika kupata ubingwa tungojee tuone tuombe salama
ReplyDeleteDo 90 no single shot on target Nani alikuwa anangoja Penalt?Hilo huwa hamjibu.
ReplyDelete