BAADA ya kikosi cha Azam FC kumalizana na wapinzani wao Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, kesho wanakazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Mwadui FC.
Dakika 90, Kaitaba ubao ulisoma Kagera Sugar 1-2 Azam FC ambapo nyota wao Prince Dube alipachika bao lake la nane ndani ya ligi akiwa ni kinara ndani ya kikosi hicho kwa utupiaji chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina.
Akizungumza na Saleh Jembe, Vivier Bahata, kocha msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wanaamini mchezo huo utakuwa mgumu hivyo wapo tayari kwa ajili ya ushindani ndani ya uwanja na wataingia kwa tahadhari ili wasipoteze malengo yao.
"Utakuwa ni mchezo mgumu hasa ukizingatia kwamba Mwadui FC inapambana kujinusuru kutoka kushuka daraja kutokana na matokeo ambayo wanayapata ndani ya uwanja.
"Haina maana kwamba ni timu mbaya hapana ipo vizuri hivyo nasi tutaingia uwanjani kwa tahadhari kusaka ushindi ndani ya dakika 90, mashabiki watupe sapoti," .
0 COMMENTS:
Post a Comment