March 5, 2021



NAHODHA wa Simba, John Bocco anaongoza kwa wazawa wenye mabao mengi ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa nayo tisa kibindoni pia ana pasi mbili za mabao.

Namba hiyo ya Bocco inakwenda sambamba na mshikaji wake Meddie Kagere ambaye yeye pia ametupia jumla ya mabao tisa.

Kagere ni mshambuliajiambaye anapambana kuweza kurejesha kiatu chake cha ufungaji bora ambacho alisepa nacho msimu wa 2019/20.

Wakati mabingwa hao watetezi wakiwa ni namba moja kwa upande wa kutupia mabao mengi wakiwa nayo 45 pia watengeneza mipango namba moja wanatokea Simba wakiwa na pasi tisa.

Luis Miquissone mwenye mabao matatu ana pasi tisa za mabao sawa na Clatous Chama mwenye mabao sita na ana pasi tisa za mabao.

Didier Gomes Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ushindi ndani ya uwanja unamtegemea kila mchezaji hivyo kila mmoja ana kazi ya kupambana kufanya vizuri.

 "Kila mchezaji ana jukumu la kupambana ndani ya uwanja ili kuipa timu ushindi, imani yangu ni kwamba kwa sasa kila mchezaji analitambua hilo na tutapambana kufanya vizuri,".

3 COMMENTS:

  1. Umeanza kifafa chako cha rekodi!
    unajua nini ndugu mwandishi na wewe ulikuwå umeweka rekodi kutubandikia msimamo wa ligi kuu hadi mara mbili kwa wiki..Sasa inapita wiki! baada ya kuona timu yako inasua sua katika ligi ukaamua kuacha kuweka msimamo wa ligi kuu.Hebu weka.

    Unajua nini cha kuandika kama unapenda rekodi!Kwa miaka 5 sasa YANGA WAMEWEKA REKODI YA KUTOIFUNGA COASTAL MKWAKWANI! ni au sare ama kufungwa..Chukua hiyo rekodi na uiweke kwenye kona ya ubongo wako!Teja wa rekodi zisizo na maana!

    ReplyDelete
  2. Utopolo hatimaye agongeka mkwakwani, dada and naye agongeka bunju mo arena

    ReplyDelete
  3. Yanga yatolewa bikira tanga na dsm

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic