March 29, 2021

 


PITSO Mosimane, Kocha Mkuu wa Al Ahly amesema kuwa anatambua uwezo wa mshambuliaji wao namba moja Meddie Kagere kwa kuwa aliwahi kuwafunga walipokutana Uwanja wa Mkapa.

Februari 12,2019 kikosi cha Al Ahly ya Misri kilipoteza pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Bao la ushindi lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 65 kwa pasi ya mzawa John Bocco liliwafanya wakwame kusepa na pointi tatu. Pia walipokutana na Simba Uwanja wa Mkapa msimu wa 2020 walifungwa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Luis Miquissone.

Kwa sasa kikosi cha Al Ahly kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kipo nafasi ya pili na pointi zao ni 7 baada ya kucheza mechi nne na kinara ni Simba mwenye pointi 10 kibindoni.

Mosimane amesema:"Simba ni moja ya timu bora na ninawatambua wachezaji wake kwa sababu nimekuwa nikiwafuatilia kwa ukaribu hivyo majina yao na uwezo wao tunawatambua.

"Kwenye mchezo ambao walitufunga ule mara ya kwanza niliutazama na niliona namna ambavyo wanafanya hivyo nina amini kwamba tukikutana nao tena utakuwa mchezo mgumu.

"Kupoteza kwetu kwao haina ubaya kwa sababu ushindi ulitengenezwa kwa mipango nasi tutapambana ili kutengeneza ushindi uwanjani kwani kila kitu kinawezekana," amesema.

Simba itamenyana na Al Ahly Aprili 9 mchezo wa Ligi ya Mabingwa ambapo itakuwa ugenini na kabla ya kuvaana na Waarabu hao wa Misri itaanza kumenyana na AS Vita ya Congo, Aprili 3, Uwanja wa Mkapa.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic