March 29, 2021

 


AMRI Said, Kocha Mkuu wa Mwadui FC amesema kuwa amechanganyikwa kutokana na kifo cha aliyekuwa Rias wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli.

Magufuli alitangulia mbele za haki Machi 17 kwa matatizo ya moyo kwa mujibu wa Makamu wake wa Rais, Samia Suluhu ambaye kwa sasa ni Rais wa Tanzania kwa mujibu wa katiba.

Akizungumza na Saleh Jembe, Said ambaye timu yake ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 24 amesema kuwa hana la kuzungumza kuhusu mpira kwa sababu ya msiba wa Magufuli.

“Kwa kweli kwa sasa sijui niseme nini, yaani naona kabisa nimechanganyikiwa kutokana na msiba wa Magufuli, siwezi kabisa siwezi kuzungumza chochote kuhusu mpira.

“Nimeamua nijipe mapumziko kwa muda na nisizungumze kuhusu mpira mpaka pale hali yangu itakapokuwa sawa ila itachukua muda kidogo kurudi kwenye hali yangu ya kawaida,” amesema Said.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic