March 6, 2021


IMEELEZWA kuwa Klabu ya Juventus ambayo inashiriki Serie A ipo kwenye hesabu za kuipata saini ya kiungo wa Chelsea, Jorginho ili awe ndani ya kikosi hicho msimu ujao.

Nyota huyo ambaye yupo mikononi mwa Thomas Tuchel ambaye ni Kocha Mkuu wa Chelsea anatajwa kuwa  kwenye hesabu za Kocha Mkuu wa Juventus, Andrea Pirlo kwenye usajili wa msimu huu.

Licha ya Juventus kumhitaji Jorginho, utakuwa ni mpango wa pili ikiwa hesabu za chaguo lao la kwanza la kuipata saini ya Manuel Locatelli ambaye ni kiungo bora ndani ya kikosi cha Sassuolo na dau lake linatajwa kuwa pauni milioni 30 kubuma.

 Hata hivyo ripoti zimeeleza kwamba Juve hawapo tayari kutoa zaidi ya pauni milioni 30 jambo ambalo limewafanya wafikirie plan B ya kumpata kiungo mwingine, jambo lililofanya jina la nyota huyo wa Chelsea kuwekwa kwenye hesabu zao za usajili.

Kwa mujibu wa Calciomercatio, Juverntus walianza kumuweka kwenye rada Jorginho tangu zama za Maurizo Sarri akiwa ni kocha mkuu jambo ambalo linawafanya wawe na uhakika wa kile ambacho wanakifanya.

 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic