March 3, 2021

 


KIKOSI cha klabu ya Yanga leo kimefanya mazoezi yao ya mwisho kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Coastal Union huku wakitamba kufanya vizuri katika mchezo huo.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa katika dimba la Mkwakwani, jijini Tanga majira ya saa 10 kamili jioni.

Yanga wametamba kuwa, ushindi wa bao 1-0 walioupata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kengold, katika michuano ya kombe la Shirikisho umezidi kuamsha ari ya kushinda mchezo wa kesho.

Akizungumzia maandalizi yao kuelekea mchezo huo, Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amewaomba Wanayanga kujitokeza kwa wingi, ili kuwapa sapoti wachezaji wa kikosi hicho.

“Kikosi chetu kimekamilisha mazoezi ya mwisho leo kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Coastal Union.

“Ni wazi ushindi tulioupata katika mchezo uliopita dhidi ya Kengold kwenye michuano ya kombe la FA, umezidi kutupa ari ya kufanya vizuri kwenye mchezo huu,”

5 COMMENTS:

  1. Coastal tandika hap malalamiko fc ili wanitoe vizuri kwenye ligi

    ReplyDelete
  2. Tawi lenu mikia aka paka mweusi

    ReplyDelete
  3. TFF iwamilike fujo za makomandoo wao

    ReplyDelete
  4. Utopolo leo presha kama yote... Yanagonga yanarudi. Kichapo kinawahusu leo wakijitahidi saaana wanapata sare

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic