March 3, 2021

 

BAADA ya klabu ya Simba Queens, leo kumtambulisha rasmi muigizaji, Yvonne Cherrie maarufu ‘Monalisa’ kuwa msemaji wa kikosi hicho, tayari msemaji huyo ameanza mikwara ya hatari.

Monalisa amekaribishwa rasmi ndani ya Simba Queens na mlezi wa klabu hiyo, Fatema Dewji.

Akizungumza baada ya uteuzi huo Monalisa alisema: “Mimi ni Simba jike (Simba Queen), ahsante Mungu, ahsante wanasimba wote na mwisho Ahsante mama mlezi wa Simba Queens, Fatema Dewji kwa kunikabidhi kijiti cha kuisemea Timu yangu pendwa.

“Sasa ni muda wa kazi, muda wa kuionesha dunia ukubwa wa Simba, mwisho naomba kutoa tangazo rasmi ya kwamba kila binti/Mwanamke nchi hii ni shabiki wa Simba Queens,”

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic