March 28, 2021



KOCHA msaidizi wa Simba Queens, Sophia Msety (Matty Msetty) ameitaja timu ya Daraja la Kwanza ya Fesh FC, kuwa itakuja kutisha kwenye soka la wanawake nchini kutokana na misingi bora inayojengwa na viongozi wa timu hiyo.

Msetty ambaye anajifananisha na kocha Manchester City, Pep Guardiola akijiita Mattidiola, amesema kuwa kuwa timu hiyo ina wachezaji wanaochipukia kwenye soka, lakini misingi wanayopitia ni ya kisasa na baada ya muda mfupi watakuwa na timu imara zaidi.

“Hii timu ni changa na ina wachezaji wengi ambao wanachipukia, hivyo baada ya muda mfupi watakuja kukaa sawa na kuwa timu bora Tanzania, hiyo ni kwa sababu ya misingi yake ambayo viongozi wanajaribu kuwatengenezea vijana hao,” amesema Mattidiola.

Fesh jana Jumamosi iliyopita walikuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Ilala Queens, ambayo itashiriki daraja la kwanza pia, mchezo uliochezwa Tanganyika Packers Dar wakifungwa mabao 3-1.

 


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic