March 28, 2021

 

KOCHA msaidizi wa kikosi cha Azam FC Vivier Bahati amefunguka kuwa, hesabu zao benchi la ufundi likiongozwa na George Lwandamina za kuwania ubingwa wa msimu zimeongezeka na kuwa kali zaidi baada ya kuhimarika kwa viwango vya wachezaji wake. 

Vivier alisema mara zote alizozungumza na Lwandamina ameonekana kuwa ni mtu ambaye anauhitaji zaidi ubingwa wa msimu huu, ili kurejesha heshima ya kuitwa mabingwa waliyoikosa kwa miaka saba sasa.

Baada ya kutoa mapumziko mafupi hatimaye kikosi cha Azam FC kimerejea mazoezini rasmi wakijiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo utakaochezwa April 6,2021 katika uwanja wa Azam Complex.

Azam wamerejea kambini huku baadhi ya nyota wao kadhaa wakiwa kwenye majukumu yao ya timu za taifa kuwania tiketi ya kufuzu Afcon 2021 nchini Cameroon.

Akizungumzia mipango yao Bahati: “Ukitazama pengo la pointi baina yetu na wanaoongoza utaona siyo kubwa sana na ndiyo maana hata kocha wetu amekuwa akipiga hesabu za kutwaa ubingwa.

"Baadhi ya wachezaji wetu ambao walionekana kuwa chini kidogo, sasa wanaonekana kuwa imara zaidi. Nadhani hiyo itasaidia sana.”

Azam wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 44, wakipitwa na Simba pointi mbili, wakizidiwa alama sita na kinara Yanga ambao inalingana nao michezo 23, Simba wakiwa na mechi 19.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic