MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga Princess, Aisha Masaka amefunguka kuwa, malengo yake makubwa ni kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kama ilivyokuwa kwa Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ aliyetimkia nchini Morocco.
Akizungumzia kuhusiana na malengo yake, Masaka amesema: “Mchezo wa soka umezidi kukua na kuwa biashara kubwa katika maeneo mbalimbali duniani, na kila ndoto ya mchezaji ni kuona anapata masilahi mazuri na kucheza soka la ushindani.
“Hivyo natamani nami nifikie kule ambako wamefika wenzangu ikiwemo Gaucho,”
Masaka ameifungia Yanga mabao 20,
kwenye Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu
0 COMMENTS:
Post a Comment