FT: Tanzania 1-0 Libya
Zinaongezwa dk 3
Dakika 90 Libya wanapata faulo
Dakika ya 89 Nyoni anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 82 Manula anapewa huduma ya Kwanza
Dakika ya 79, Libya wanapata kona tatu ndani ya dakika moja
Dakika ya 78 Kibabage anafanya jaribio linakwenda nje ya lango
Dakika ya 75 Chilunda anaotea
Dakika ya 72 Himid anaingia kuchukua nafasi ya Fei Toto, Dilunga anatoka anaingia Abdul
Dakika ya 67 Manula anaokoa hatari nyingine tena, safu ya ulinzi ya Stars imekuwa ikipitika katika dakika za muda huu
Dakika ya 64 Manula anaokoa hatari ndani ya 18 na kuifanya iwe kona haileti matunda
Dakika ya 57 Nyoni anamchezea faulo mchezaji wa Libya
Dakika ya 55 Kaseke anatoka anaingia Chilunda, Nondo, anachukua nafasi ya Mkude , Msuva anatoka anaingia Lyanga
Dakika ya 54 Msuva anachezewa faulo mwamuzi anapeta
Dakika ya 52 Manula anaokoa hatari baada ya mabeki kuwaacha wachezaji wa Libya kuamua wanavyotaka ndani ya 18
Dakika ya 48 mchezaji wa Libya anachezewa faulo ndani ya 18 na beki wa Stars, Mwamuzi anapeta
Dakika ya 48 Mkude anampelekea Fei Toto
Dakika 47 Libya wanafanya jaribio kwa Manula linakwenda nje kidogo ya uwanja
Dakika ya 46 Libya wanapata kona haizai matunda
Kipindi cha pili kimeanza
Mapumziko:-Uwanja wa Mkapa
Tanzania 1-0 Libya
Uwanja wa Mkapa
Dakika ya 45+1 Msuva goooooal
Zinaongezwa dakika 2
Dakika ya 45 Libya wanapeleka mashambulizi kwa Manula
Dakika ya 44, Mkude anaonyeshwa kadi ya njano, Fei Toto anaotea
Dakika ya 38 Samatta anafanya jaribio zuri linakwenda nje kidogo ya lango
Dakika ya 35 Kaseke anachezewa faulo na kipa wa Libya wakati huu anapewa huduma ya kwanza
Dakika ya 33 Kibabage anakosa nafasi ndani ya 18
Dakika ya 29 Dilunga anapiga kona inaokolewa na kipa wa Libya.
Dakika ya 27 Manula anaokoa hatari
Dakika ya 25, Simon Msuva anakosa nafasi ya wazi ndani ya 18.
Dakika ya 24, Kaseke anachezewa faulo.
0 COMMENTS:
Post a Comment