March 28, 2021

 


SELEMAN Matola, Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania,  Taifa Stars amesema kuwa walishindwa kupata matokeo mazuri mbele ya Equatorial Guinea baada ya kushindwa kutumia nafasi walizopata.


Stars ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea Machi 25 na leo ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Libya, Uwanja wa Mkapa.


Kupoteza mbele ya Equatorial Guinea kumeyeyusha matumaini ya Stars kufuzu Afcon, nchini Cameroon hivyo leo wanacheza na Libya ambayo nayo haijafuzu Afcon.


Matola amesema:" Tunajua kwamba Watanzania wanapenda kuona timu inapata matokeo mazuri ila tulishindwa baada ya kushindwa kutumia nafasi chache ambazo tulipata.


"Makosa tumeyafanyia kazi tunaamini leo tutapambana kupata ushindi mbele ya Libya hivyo dua muhimu kwani wachezaji wapo tayari," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic