KIUNGO Carlos Carlinhos raia wa Angola amebakiza dakika 90 kurudi uwanjani kwenye mechi za Yanga baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja ambayo itamfanya akose mechi tatu mfululizo kwa mujibu wa kanuni zinazotumika kuendesha Ligi Kuu Bara.
Kadi hiyo alionyeshwa Februari 27, Uwanja wa Uhuru baada ya kuonekana akimpiga ngumi Boniphace Mwanjode, beki wa Klabu ya Ken Gold inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-0 Ken Gold na bao lilipachikwa kimiani na mshambuliaji wao Fiston Abdulazack kwa mkwaju wa penalti.
Mpaka sasa tayari amekosekana kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180, ilikuwa mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani wakati timu yake ikipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na ile ya sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania.
Mchezo wao ujao ambao ni wa Kombe la Shirikisho dhidi Tanzania Prisons utakuwa ni wa mwisho kwa raia huyo wa Angola kukaa jukwaani akitumikia adhabu hiyo.
Kwa sasa kikosi kipo kambini Kigamboni kikiendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.
Ipo chini ya mzawa Juma Mwambusi ambaye ni Kaimu Kocha Mkuu ambaye amebeba mikoba ya Cedric Kaze raua wa Burundi ambaye alichimbishwa Machi 7.
0 COMMENTS:
Post a Comment