WAKATI wachezaji wa Simba wakiongozwa na Kocha Mkuu, Didier Gomes leo wakiendelea na mazoezi Uwanja wa Mo Simba Arena kwa ajili ya mchezo wa wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, dhidi ya AS Vita, majina matatu yanawania tuzo.
Wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Machi inayodhaminiwa na Emirates Aluminium Profile ni Luis Miquissone ambaye ni kiungo mshambuliaji, Joash Onyango ambaye ni beki wa kati na Aishi Manula kipa namba moja.
Tuzo ya kwanza ya mwezi Februali Luis wengi wanapenda kumuita Konde Boy alisepa nayo na sasa yupo tena kwenye mchakato wa kuwania tuzo hiyo.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mchakato wa kumpata mchezaji bora unakwenda na kitu kinachokwenda data za kiujumla jambo ambalo linatoa nafasi kwa kila mchezaji kupata nafasi ya kuwa kwenye hesabu za kutwaa tuzo.
"Kila mchezaji ana nafasi ya kutwaa tuzo kwa kuwa tuna mtaalamu ambaye anafuatilia kila kitu, kuanzia mabeki, washambuliaji mpaka viungo hapa hii sio tuzo ya washambuliaji pekee.
"Nadhani mashabiki wao jukumu lao ni kupiga kura hivyo watapewa maelekezo na ufafanuzi wa sababu za wachezaji kuwa kwenye mchakato huo na kazi ni kwao kumpigia mchezaji wanayemtaka kupitia tovuti yetu ya Simba," .
Vitu kama hivi ndivyo vinachojenga umoja na mahaba baina ya waungwana na kujiona kila mmoja anathaminiwa
ReplyDelete