March 29, 2021

 


WAKATI akiwa madarakani, aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli alikuwa akipenda pia kufuatilia michezo ndani ya ardhi ya Tanzania na nje pia.

Kwa msimu wa 2016/17 timu tatu bora ndani ya Ligi Kuu Bara, Magufuli aliweza kushuhudia Klabu ya Yanga ikitwaa ubingwa baada ya kukusanya jumla ya pointi 68.

Msimu huo jumla timu tatu za juu zilikusanya pointi 189. Wadau na familia ya mpira itaendelea kumuenzi Magufuli ambaye alitangulia mbele za haki Machi 17 na kupumzishwa kwenye makazi yake ya milele Machi 26, kwenye makaburi ya familia ya Magufuli, Chato. 

Yanga ilishinda mechi 21, sare 5 ilipoteza mechi 4. Safu ya ushambuliaji ilifunga mabao 57 na ile ya ulinzi iliruhusu mabao 14.

Kwa upande wa nafasi ya pili, Simba ilikuwa hapo baada ya kukusanya pointi 68, ilishinda mechi 21, sare 5 na ilipoteza 4. Ilifunga mabao 50 ilifungwa mabao 17.

Simba ilipotezwa na Yanga kwa idadi ya mabao ya kufunga ambapo ilitofautiana kwa mabao 7, na wakati huu uliubuka ule mgogoro wa pointi tatu za Fakhi wa Kagera Sugar ambazo Simba walishindwa baada ya rufaa kukatwa na wapinzani wao.

Namba 3 ilikuwa kwa Kagera Sugar, ilikusanya pointi 53, ilishinda mechi 15, sare 8, ilipoteza 7, Safu ya ushambuliaji ilifunga mabao 33 na ile ya ulinzi iliruhusu mabao 26 zote zilicheza mechi 30.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic