March 28, 2021

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Rwanda anayekipiga katika klabu ya APR, Jacques Tuyisenge amesema kuwa anatamani kucheza katika Ligi Kuu ya Tanzania na kuvutiwa na timu za Simba na Yanga.

Tuyisenge amewahi kucheza na wachezaji Meddie Kagere na Francis Kahata katika klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya, ambapo wacheza hao kwa sasa wanakipiga katika klabu ya Simba.

Akizungumzia uwezekano wake kucheza ndani ya Ligi Kuu Bara, Tuyisenge amesema: “Nimecheza katika ligi kama ya Rwanda, Kenya na Angola, natamani kuona pia nikipata nafasi ya kucheza katika ligi ya Tanzania ambayo imekuwa maarufu katika ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki.

“Ushindani mkubwa uliopo kati ya klabu za Simba na Yanga ni chanzo cha ligi ya Tanzania kuchangamka, kutokana na upinzani unaopatikana katika ligi husika, hivyo hata Tanzania Simba na Yanga zinachangia kwa kiasi kikubwa ligi kuwa yenye mvuto,”

Katika dirisha kubwa la usajili la msimu uliopita, Tuyisenge alikuwa akihusishwa kujiunga na Yanga lakini dili hilo halikufanikiwa kukamilika.

4 COMMENTS:

  1. Huyu si alikuwa anaringa kipindi kile? Kachoka ndio anataka kuja huku kutuibia hela? Wampotezee tuu hana jipya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kabisa nikumpoteea kabisa, kawa galasa ndo aje TZ

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic