March 29, 2021


KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, (Beach Soccer), Boniphace Pawasa amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho Machi 30 dhidi ya Burundi.


Pawasa ana kazi ya kukiongoza kikosi hicho kwenye mechi mbili za kufuzu AFCON dhidi ya timu ya taifa ya Burundi, Machi 30 na ile ya pili itachezwa Aprili 3, zote zitachezwa Dar, Uwanja fukwe za Coco Beach.


Akizungumza na Saleh Jembe, Pawasa amesema kuwa wanatabua mchezo utakuwa mgumu ila watapambana kupata ushindi kwenye mchezo huo.


“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Burundi, na wachezaji wanatambua kwamba wana kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wetu dhidi ya Burundi.


“Muhimu kupata ushindi kwani hakuna namna nyingine ambayo itatufanya tuwe na furaha sisi benchi la ufundi na wachezaji bila kusahau mashabiki kiujumla," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic