March 17, 2021

 


SHABAN Kazumba, kocha msaidizi wa Tanzania Prisons amesema kuwa wapinzani wake ambao watakutana nao uwanjani ni lazima wajipange kukutana na pira gwaride kwa kuwa huo ni mwendo wao kwa sasa.

Prisons inashikilia rekodi ya kuwapa tabu vigogo wa Bongo, Yanga na Simba ambapo timu hizo mbili zote hazijaambulia ushindi kwenye mechi mbili ambazo walikutana nao.

Simba zama za Sven Vandenbroeck ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na ule wa pili zama za Didier Gomes, ngoma ilikuwa 1-1 na kwa Yanga mechi zote mbili ngoma ilikuwa 1-1.

Kazumba amesema:”Sisi tunacheza kwa afya na mwendo wetu ni pira gwaride, tukikutana na timu za jeshi hapo kidogo huwa tunakwenda nao sawa kwa kuwa nao wanacheza aina ya mpira wetu ila wapinzani wetu lazima wajipange kwa pira gwaride,”.

Prisons ipo nafasi ya 8 ina 31 baaada ya kucheza jumla ya mechi 23.

3 COMMENTS:

  1. Kocha mzima unajobunia mpira wa kihuni?

    ReplyDelete
  2. Ifike mahali timu za majeshi zizuiliwe kushiriki ligi zote zinazosimamiwa na tff. Mpira ni burudani na sio vita. Yaani watu wazima na akili zao wanajivunia vita kwenye mpira? Shame on them

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic