KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa anaamini nyota wa kikosi hicho ambao ni Carlos Carlinhosraia wa Angola pamoja na Yacouba Sogne raia wa Burkina Faso, watarejea kwenye kasi ya kucheka na nyavu.
Mwambusi yupo na wachezaji wake katika kijiji cha Avic Town Kigamboni ambako amejichimbia na wachezaji wake kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu Bara na ile ya Kombe la FA.
Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama na kikosi cha Yanga kimekusanya pointi zake 50 baada ya kucheza mechi 23.
Mwambusi, ameweka wazi kuwa, sasa mambo kwa viungo washambuliaji wake, Yacoub na Carlinhos, tangu wameanza mazoezi wamekuwa wakionyesha hali ya kupanda kwa viwango vyao jambo linalompa matumaini ya kuja kufanya maajabu ligi ikianza.
“Tangu nimeingia kambini Jumatatu, baada ya kupumzika kwa takriban siku tatu ulipotokea msiba wa Hayati Rais Joseph Magufuli,
nashukuru sana wachezaji wangu viwango vyao vimezidi kuwa juu, ambapo ukiachana na wengine kwa sasa Carlinhos na Yacouba kwa pamoja wameiva.
“Ni matumaini yangu kama ligi ikirejea watakuja kufanya maajabu kufuatia hali zao za kuendana na program za mazoezi kukubali, kwani kila aliyekaribu nao anaweza kuthibitisha kuwa sasa vijana hawa wameiva na kwamba mimi naendelea kuwaombea kwa Mungu hadi ligi itakaporudi waje kuwa tishio zaidi,” amesema Mwambusi.
Chanzo: Championi
Mwambieni Mwambusi apunguze maneno asije jutia kauli zake mwenyewe
ReplyDelete