KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, (Beach Soccer), Boniphace Pawasa amesema kuwa amewekeza nguvu kubwa kwa sasa kwenye mipira iliyokufa ili vijana wake wawe imara zaidi.
Pawasa ana kazi ya kukiongoza kikosi hicho kwenye mechi mbili za kufuzu AFCON dhidi ya timu ya taifa ya Burundi, Machi 30 na ile ya pili itachezwa Aprili 3, zote zitachezwa Dar.
Akizungumza na Spoti Xtra, Pawasa alisema kuwa maandalizi ya kawaida yamekamilika kwa asilimia 100 kilichobaki ni kukamilisha maandalizi ya mwisho kwa kuwabadilishia mbinu za kusaka ushindi kabla ya mchezo.
“Kwa upande wa maandalizi ya wachezaji yamekamilika kilichobaki ni kuweka sawa mambo madogo ambayo yamekuwa yakikosekana, hasa kwenye upigaji wa mipira iliyokufa pamoja na kumalizia mipango mbinu ambayo itatupa matokeo.
“Imani yetu ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya hasa ukizingatia kwamba tupo nyumbani hatuna haja ya kuwa na hofu. Malengo yetu ni kuona kwamba yanatamia kwa kushinda mechi zetu,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment