March 28, 2021


 JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha wa Klabu ya Yanga amesema kuwa suala la wao kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa sasa ni jambo linalosubiri muda.

Ikiwa imecheza mechi 23 inaongoza ligi na imekusanya juma ya pointi 50 kibindoni.

Watetezi wa taji hilo ambao ni Simba wapo nafasi ya pili na pointi zao ni 46 baada ya kucheza mechi 20.

Tayari kikosi cha Yanga kimeanza mazoezi Kigamboni kwa ajili ya mechi za ligi pamoja na zile za Kombe la Shirikisho.

Mwambusi amesema:"Natambua kwamba mashabiki pamoja na wachezaji wanahitaji kuona timu inashinda na kutwaa taji la ligi hilo lipo wazi na tunaamini kwamba tutapambana kufikia lengo hilo.

"Kwa sasa ni suala la muda kwa kuwa bado ligi inaendelea kwa mechi zetu ambazo zimebaki tutapambana kupata matokeo chanya,". amesema.

Yanga inawania mataji mawili msimu huu ambapo ni lile la Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho na yote bingwa mtetezi ni Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic