WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba, Jumamosi ya Machi 6, mwaka huu, kwa mara nyingine watatupa karata yao ya tatu katika hatua ya makundi kwa kucheza na timu ya Al Merrikh ya Sudan.
Machi 6 yenyewe ni kesho ambayo inasubiliwa kwa shauku na mashabiki wengi Tanzania na nje ya Tanzania huku Visit Tanzania ikizidi kupasua anga.
Kwa namna ambavyo ushindani ulivyo na aina ya mchezo wenyewe kuwa ni wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika zitakuwa ni dakika 90 za ushindani mkubwa.
Mchezo huo, utapigwa siku ya Jumamosi, Sudan ukiwa ni mchezo wa pili kwa Simba kucheza ugenini katika hatua hiyo. Ule wa awali walicheza pale DR Congo dhidi ya AS Vita na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mpaka sasa Simba katika Kundi A wao ni vinara wakiongoza kwa pointi sita baada ya kushinda michezo yake miwili ya awali akimfunga Al Ahly(1-0) na As Vita(0-1) na safari hii atacheza na mpinzani wake watatu.
Ushindi ambao Simba walipata katika michezo ya awali ni wazi sio tiketi ya moja kwa moja wao kusema watashinda mbele ya Al Merrikh hivyo, wanatakiwa kujipanga kweli katika hilo kwa kuhakikisha wanarejea nyumbani na pointi tatu.
Simba inaenda kucheza mchezo wake wa tatu huo, lakini, itakumbana na ugumu kutoka kwa wapinzani wao ambao tayari wana maumivu makali na wanamachungu kutokana na vipigo ambavyo tayari wameambulia katika michezo ya awali ilipocheza dhidi ya As Vita na Al Alhy, hivyo Simba inatakiwa kujipanga.
Kwa sasa hakuna asiyefahamu ubora na uimara wa kikosi cha Simba, lakini wanapoenda kupambana Sudan wanatakiwa kwenda kwa tahadhari kubwa kwani huu ni moja kati ya mchezo mgumu ambao wanaenda kukutana nao tofauti na wengi ambavyo wanaichukulia Al Merrikh.
Nidhamu, kufuata maelekezo ya kocha au kile ambacho watakuwa wanaelekezwa kinatakiwa kukaa vizuri katika vichwa vya wachezaji wa Simba wanatakiwa kucheza kwa umakini na wasijiamini sana sababu huu ni mpira lolote linaweza kutokea kwao kama wasipokuwa makini.
Tunafahamu kuwa siku zote mpira una matokeo ya aina tatu, lakini bidii pia ndani ya uwanja inaweza kubadili mambo, kwani kila hamu ya mwanasimba na watanzania kwa ujumla ni kuona timu hiyo inaendelea kupata matokeo bora na kuendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania vyema katika michuano hiyo mikubwa.
Hivyo hawa Wasudan wasidharauliwe bali wanatakiwa kuangaliwa kwa umakini na tahadhari kubwa na pia tayari watakuwa wamewasoma vizuri Simba katika michezo iliyoita, ingawa na Simba nao tayari wamefanya hivyo, soka la nidhamu linatakiwa kuzingatiwa kwa kiasi kikubwa.
Pia wachezaji wa Simba wanatakiwa wasijisahau bali wazingatie nidhamu wajitume na wasijiamini sana wakapatiliza na kuweza kuharibu mambo, zaidi wapambane kupata matokeo na kuendelea kuandika historia bora ndani ya michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ile rekodi ya hivi karibuni ya kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, safari hii wanatakiwa kuifuta na kwenda mbali zaidi kwa kufika hatua ya nusu fainali na hata ikiwezekana fainali kabisa na kuweka historia bora kabisa kuwahi kutoka kwa timu za upande wa Afrika Mashariki na Kati.
Una uhakika gani hayo mabao unayosema hayatajirudia wewe ni Mungu,alafu kitu kingine Ushauri wako ni mzuri lakini hicho unachowashauri Simba wao wanaoijua labda ungetoa Ushauri mwingine
ReplyDeleteSIMBA ALISHAFUNGWA HAPO HAPO NA EL MEREIKH, UNADHANI WAO WAJINGA? WANAKWENDA NA KOCHA AMBAYE ANAIJUA HIYO TIMU. UNADHANI HUYO OCHA MJINGA? SIMBA WANATAKA KUJIHAKIKISHIA KUFUZU KATIKA MECHI YA KESHO
ReplyDeleteMO KASEMA MALENGO YA TIMU NI KUCHEZA NUSU FAINALI BASI, NA SIO FAINALI, GOMEZI KAPEWA KAZI YA KUIPELEKA SIMBA ROBO FAINALI. INA MAANA SUALA LA KUFUPITA KWENDA NUSU NDIYO MKAKATI WA MWISHO NA SIO ZAIDI YA HAPO...UNADHANI TIMU KUCHEZA FAINALI NI KAZI RAHISI?
ReplyDeletesimba anashinda hakuna wasiwasi....ingawa mimi ni mpenzi wa Yanga....hii Simba itashinda mechi zote mbili nyumbani na ugenini kwakuwa el-merreikh sio timu bora....ina mapungufu mengi mno
ReplyDeleteAl wewe ni wa aina yake, uwe Yanga lakini unazungumza hayo, wewe ni mkweli kwelikweli
ReplyDelete