April 17, 2021


KUELEKEA katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya watani wa jadi Yanga, Kariakoo Dabi unaotarajiwa kuchezwa Mei 8, Simba wameanza kupiga hesabu ndefu kwa kutuma mkwara kwa wapinzani wao.

Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba na kuwafanya wagawane pointi mojamoja. 

Mabao yote yalifungwa na wageni ambapo kwa Yanga alikuwa ni Michael Sarpong raia wa Ghana  aliyefunga kwa penalti na kwa Simba alikuwa ni Joash Onyango raia wa Kenya.

Kupitia Ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba wameandika kuwa, hizi mechi nyingine ni kama Warm Up ila shughuli yenyewe itakuwa ni Mei 8.

Simba kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu ikiwa imecheza jumla ya mechi 21 ina kibarua cha kusaka pointi tatu kesho mbele ya Mwadui, kesho Aprili 18, Uwanja wa Karume.

Watani zao wa jadi, Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 24 na leo wana kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Biashara United.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic