April 15, 2021


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa utajiuliza wapi ambapo umekuwa ukikosea kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 17.

Yanga kwenye mzunguko wa pili baada ya kucheza mechi 7 imeshinda mchezo mmoja, sare tano na imepoteza mchezo mmoja.

Kwenye msimamo ukitazama kwa sasa bado ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 24 nafasi ya pili ipo mikononi mwa watani zao wa jadi Simba wenye pointi 49 baada ya kucheza mechi 21.

Mchezo wao uliopita walipokutana na Biashara United, Uwanja wa Karume Mara, Yanga ilishinda bao 1-0 ambalo lilifungwa na Michael Sarpong kwa pasi ya Ditram Nchimbi.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa mchezo wa mpira umekuwa na matokeo ambayo hawatarajii ila watajiuliza wapi ambapo wamekuwa wakikosea mbele ya Biashara United.

"Tutajiuliza wapi ambapo tumekuwa tukikosea mbele ya Biashara United, siku ya jumamosi na hili linawezekana kwetu pamoja na mashabiki.

"Wito ni kwamba mashabiki wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Mkapa kushuhudia burudani na namna ambavyo tutasaka pointi tatu kwa kuwa kila kitu kipo sawa," amesema.

2 COMMENTS:

  1. Kocha ameshindwa kuwafanya wachezaji wawe wepesi. Ni wazito mnoo.

    ReplyDelete
  2. wameona biashara haipo imara wameanza kujisifu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic