April 16, 2021

 


KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu Bara

utakaopigwa leo Ijumaa, timu ya KMC

imewataka Gwambina FC kuwauliza Yanga kitu

gani walichokutana nacho Jumamosi iliyopita

kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar wakati

walipokutana nao na mchezo kumalizika kwa

sare ya bao 1-1.

 

Timu hizo zinatarajiwa kukutana leo kwenye

  Uwanja wa Uhuru jijini Dar, ambapo Gwambina

katika mchezo uliopita walisepa na pointi tatu mbele ya Coastal Union kwa mabao 4-0.

 

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema:

“Tunawasalimu kwa jina la KMC, pia

tuwakaribisha Gwambina kwenye Uwanja wa

Uhuru ambao ni maalum kwa ajili ya machinjio

yetu.

 

“Hali ya kikosi iko vizuri ila itakosa huduma ya

wachezaji watatu wenye majeraha ambao ni

David Bryson, Kenny Ally na Sudi Dondola

lakini wengine wote wapo fiti.

 

“Hakuna timu ambayo inatoka mkoani ikapata

matokeo mbele yetu kwenye uwanja wa

machinjio, kama hawaamini wawaulize wenzao

Namungo, Ruvu Shooting, Kagera Sugar na

zingine.

 

“Tunaendeleza pira spana, pira kodi, pira

mapato, wasije wakasahau njia waliyokuja

nayo, hivyo wajipange kisaikolojia kwani cha

muhimu kwetu ni lazima tuvune pointi tatu.

 

“Gwambina wanapaswa kuwauliza Yanga kitu gani ambacho walikutana nacho usiku wa

Jumamosi, nadhani walilala na viatu, kwa hiyo

na wao wajipange vizuri,” amesema Christina.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic