April 16, 2021


MTATHIMINI viwango wa timu ya Simba,

Culvin Mavhunga amefunguka kuwa kwa sasa

akili yake ipo kwenye mechi za kimataifa kuona

ni timu gani ambayo itapangwa kucheza na

Simba kwenye hatua ya Robo Fainali ili aweze

kuingia chimbo na kusaka mafaili yao.

 

Simba imekuwa kwenye kiwango bora katika

michuano ya kimataifa huku nyuma ya pazia

kazi kubwa ikifanywa na Mzimbabwe huyu ambaye alijiunga na Simba, Januari na tangu

amejiunga na timu hiyo imekuwa kwenye

kiwango bora.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, juzi

Jumatano kwenye mchezo ambao Simba

waliibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya

Mtibwa Sugar, Mavhunga alisema: “Kwa sasa tuna michezo kadhaa ya ligi ambayo ninaamini tutazidi kufanyia vizuri, lakini kwa sasa nimejikita zaidi kuwasoma wapinzani wetu ambao tunatarajia kukutana nao kwenye hatua ya Robo Fainali ya Caf kuona tutaingia na staili gani.

 

“Jambo la kufurahisha ni kuwa tutaanzia

ugenini, hivyo nina imani itakuwa rahisi kwetu

kwenye mchezo wa marudio ambao tutakuwa

nyumbani, kazi yangu kubwa ni kuhakikisha

naandaa taarifa ambayo inakwenda

kumrahisishia kazi mwalimu.”

 

Simba inatarajia kukutana na MC Alger, CR

Belouizdad au Kaizer Chiefs kwenye hatua ya

Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa ambapo droo

ya Robo Fainali inatarajiwa kupangwa Aprili 30,

2021.

 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic