April 16, 2021


UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema kuwa, upo kwenye mipango madhubuti ya kufanya usajili mkubwa katika dirisha la usajili la mwezi Juni mwaka huu kwa kuleta majembe mapya ya kazi, na kuwaondoa baadhi ya nyota ambao wanaonekana kuwa na mchango mdogo kwenye kikosi hicho.

Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha Yanga ambao inatajwa wapo kwenye hatari ya kuachwa ndani ya kikosi hicho ni washambuliaji Michael Sarpong, Fiston Abdoul Razak na Ditram Nchimbi ambao kwa ujumla wao wamefunga mabao sita tu kwenye ligi mpaka sasa.

Katika siku za hivi karibuni Yanga wameonekana kukosa makali, hasa katika safu yake ya ushambuliaji ambapo licha ya kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zao 51, kikosi hicho kimepata ushindi mmoja pekee kati ya michezo saba iliyopita imefungwa mechi moja na kutoa sare michezo mitano.

Akizungumzia hali ya kikosi chao, Kaimu Katibu Mkuu wa ya Yanga, Haji Mfikirwa amesema ni lazima klabu hiyo ifanye usajili mkubwa katika dirisha la mwezi Juni, ili kuboresha maeneo yanayoonekana kuwa na mapungufu.

“Ni kweli kama uongozi tunajua wazi kuwa licha ya ubora wa wachezaji tulionao, kikosi chetu kitalazimika kufanya usajili mkubwa katika dirisha la usajili la mwezi Juni mwaka huu, ili kufanya maboresho katika baadhi ya maeneo ambayo yameonekana kuwa na mapungufu ikiwemo nafasi ya ushambuliaji.

“Tunatarajia kusajili majina mapya makubwa kwenye usajili wa dirisha kubwa, lakini pia tutaachana na baadhi ya wachezaji ambao wanaonekana kutokidhi mahitaji ya kikosi chetu. Yanga ni timu kubwa na sifa ya timu kubwa yoyote ni lazima ihakikishe inafanya usajili hivyo kama uongozi tumejidhatiti katika hilo.”

 

7 COMMENTS:

  1. Makocha mawakala ndio wanaochagua wachezaji wabovu wanaowapa thamani kubwa kuliko uhasilia ili wapate kitu kidogo

    ReplyDelete
  2. Tumechelewa na tena sana. Wezetu wanajitayarisha kuchukuwa ubingwa wa klabu bingwa wa Africa na sisi bado tunaangushwa na timu zinazokaribia kushuka daraja. Kwanza tutafute kinachoytuangusha kabla ya yote na sio kudanganyana kusik na sababu. Tujiulize kwanza wakowapi nyota wetu kiasi watatu au wane wamepotelea wapi ambao hatuwaoni na nini sababu ya kutoweka

    ReplyDelete
  3. Ushauri wangu kwa Yanga ni kwamba wasikurupuke hata kidogo kwenye dirisha kubwa la usajili.Inabidi scouting ya wachezaji isifanywe na mawakala wapiga madili.Inabidi team ikimtaka mchezaji records ziwe wazi kwenye team husika ikiwezekana hata team ya taifa amefanya Nini.Sidhani team kubwa Kama yanga itakosa mtu hata wa kuangalia clip za mchezaji wanayemtaka au hata kumsoma kwenye weekpedia amefanya kitu gani ili wasiingizwe Chaka.Tunataka wachezaji wanaojulikana kwa takwimu Bora Kama Joash Onyango,Chama,Luis na si Kuja kwa trial.Hata Peter Muduwa beki was team ya Taifa ya Zimbabwe anaweza kuwasaidia kwenye defence ambayo imekuwa mbovu.Jambo la mwisho waupuke kusajili kwa influence ya kukomoana kwamba team Fulani inamtaka ngoja tuwakomoe.Vilevile waupuke waandishi uchwara wanaowapamba wachezaji wa kusajiliwa kwa sifa za uongo mtupu.Vilevile waache fukuzafukuza ya makocha na kumpangia kocha bench la ufundi.Kocha akija aje na bench lake au apendekeze mwenyewe Kama vilabu vikubwa Africa vinavyofanya mfano Pitso alipoenda Alhaly alienda na benchi lake la ufundi alilokuwa nalo Mamelod Sundown.Kwa ushauri wangu huo watafika mbali na mwisho kocha asiingiliwe majukumu yake kwamba mpange huyu au huyu asicheze,atapanga team kulingana na juhudi na nidhamu mazoezoni Kama anavyofanya Gomez was Simba hakuna Cha Mkude Wala Boko ni juhudi zako tu ndizo zinazokupa first eleven

    ReplyDelete
  4. Naona akili imewaingia sio hujuma tena bali uwezo mdogo wa wachezaji wenu ila mkivunja nao mkataba mkumbuke kuwalipa maana Tambwe hadi leo hamjamlipa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tupe anwani ya baba yako tupeleke fedha kwake atulipie

      Delete
  5. Onyango hamna kitu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic