ACHANA na ushindi wa mabao 5-0 walioupata
Simba, juzi katika mchezo dhidi ya Mtibwa
Sugar, jambo la ziada ni kwamba ushindi huo
umewafanya nyota wawili wa kikosi cha Simba,
Meddie Kagere na Clatous Chama kuandika
rekodi ya aina yake kwenye Ligi Kuu Bara
(VPL).
Katika mchezo huo wa juzi nyota hao wawili
walihusika katika mabao manne ambapo,
Kagere alifunga mabao mawili huku Chama
yeye akifunga bao moja na kuasisti bao moja.
Kutokana na mabao hayo Chama sasa
ameivunja rasmi rekodi yake ya msimu uliopita
ambapo kwenye Ligi Kuu Bara pekee msimu huu, Chama amehusika kwenye mabao 17
akifunga mabao saba na kuasisti mara 10.
Msimu uliopita Chama alihusika kwenye mabao
15 ya michuano yote, ambapo kwenye Ligi Kuu
Bara alifunga mabao mawili na kuasisti mara
10.
Kwa upande wa Kagere mabao yake mawili
yamemfanya afikishe mabao 56 tangu atue
ndani ya Ligi Kuu Bara, ambapo huu ni msimu
wa tatu kwake tena akifanikiwa kufunga mabao
zaidi ya 10 kwa msimu.
0 COMMENTS:
Post a Comment