April 16, 2021

IMEBAINIKA kuwa klabu ya Simba ipo katika mazungumzo na beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Tanzania na Klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco, Nickson Kibabage kwa ajili ya kumsajili kuja kukiongezea nguvu kikosi hiko msimu ujao.

Kibabage kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Youssoufia ya nchini Morroco ambapo yupo kwa mkopo akitokea Difaa ya nchini humo, ambapo alikuwa akicheza pia Mtanzania Simon Msuva kabla ya kuhamia Wydad Casablanca.

Taarifa kutoka katika chanzo chetu cha kuaminika ndani ya Simba kimetuambia kuwa ni kweli Klabu hiyo ipo katika mpango wa kumsajili Kibabage ambaye licha ya kuwa na umri mdogo, amekuwa akionyesha uwezo mkubwa hivyo wanaamini kama watampata basi atawasaidia katika mipango yao msimu ujao.

"Ni kweli Simba ipo katika mpango wa kuboresha kikosi chake, hivyo kuna wachezaji ambao wapo katika mpango wa kusajiliwa akiwemo Kibabage kwa ajili ya kuja kuongeza nguvu katika timu yetu, bado hatujakamilisha usajili wake kwa kuwa muda wa usajili bado haujafika lakini mipango ipo kwa kuwa Simba ni timu kubwa.

"Kibabage ni mchezaji mdogo lakini mwenye kipaji kikubwa, hivyo kama tutakamilisha usajili wake atatuongezea ubora katika upande wetu wa kushoto, tunajua huwa tuna michezo mingi ya nje na ndani hivyo tunaamini utakuwa msaada kwetu," kilisema chanzo hiko.

Alipotafutwa Kibabage ili kuelezea ishu hiyo amesema kuwa "Mimi simfahamu chochote kuhusu kuhutajika na Simba, hizo ni tetesi tu ambazo zinaenea lakini kwa upande wangu sijui chochote," 


 

9 COMMENTS:

  1. Juzi kwenye makala yako uliandika kwamba Tanzania hatuna hata Chama mmoja?.Nitashangaa Sana Kama Kibabage atarudi kucheza mpira bongo baada ya kuongeza bidii ili aende mbali zaidi ya hapo Morroco.Vile vile atakuja kuua kipaji chake kwa sababu sidhani Kama ataweza kumuweka bench Tshabalala au Shomary Kapombe.Dogo inabidi asaidiwe kiushauri asije akaingia Chaka na kupoteza kipaji chake kwa kuja kusugua bench Simba.Aongeze bidii ili cku moja aende Ulaya kwa manufaa ya maisha yake na team ya Taifa ili tuache kunyanyaswa na Western Africa ambazo Zina professional players wengi Ulaya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Weweeeeeee! Tshabalala anahitaji kumpata msaidizi wa uhakika na wala dogo hawezi kuja kukaa benchi kama unavo mtabiria

      Delete
    2. Kama ni kwenda Ulaya basi ni rahisi kwake kwenda Ulaya akitokea Simba kuliko akitokea hiyo timu ya Morocco, maana Simba ni kubwa kuliko hiyo timu

      Delete
  2. Mdau Rama nakubaliana na wewe kwamba Tshabalala anahitaji msaidizi lakini naona kiwango cha dogo bado kidogo halafu mdau Rodrick umesema nimpe ushauri Farid Mussa ni kweli wachezaji wetu wakina Farid, Ninja wanahitaji ushauri nasaha sana.Maana uwezi kucheza Spain kwenye mpira halafu ukatoka kuja kukaa bench Yanga.Ninja alicheza team ya Beckham Marekani halafu anakuja kusugua bench Yanga.Nilitegemea wachezaji hawa wangeenda hata Turkey, Russia au hata Northern Africa kama Tunisia, Misri maana mpira wao upo juu kuliko wetu.Mimi nafikiri sisi watoa maoni tuwasaidie kuwapa ushauri wachezaji wetu wawe wavumilivu kama Ulimwengu, Samatta, Himid Mao au Msuva

    ReplyDelete
  3. Mmmmh yaani ni kama kushuka kwenye yutong unarudi kupanda bajaji

    ReplyDelete
  4. Nikwel mimi simba damu lakini hyo dogo simushauli kabisa kuja bongo atapoteza kiwango yukowap mrisho ngasa.kiwango cha. Tshabalala nikizul sana lakini sijasikia ofa ya nje.

    ReplyDelete
  5. Kibabage nakushauri usirudi timu yoyote Tanzania, kumbuka ubora wa ligi ya Tz ni mdogo kulinganisha na Morocco.
    Hata sokoni ni rahisi kuuza mchezaji aliyetoka ligi yenye ubora kulinganisha na mchezaji aliyetoka ligi yenye ubora hafifu

    ReplyDelete
    Replies
    1. KATIKA HII TIMU HANA NAFASI. SIMBA IMETENGENEZWA KATIKA MIGUU YA AKINA ZIMBWE NA SHOMARI. AMUULIZE GADIEL MICHAEL. UWEZO WAKE HAWEZI KUWA SAWA NA ZIMBWE JR. LABDA ZIMBWE JR. AONDOKE ABAKI YEYE

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic