May 14, 2021


 IMEELEZWA kuwa kukosekana kwa vifaa muhimu kwa ajili ya mazoezi ni sababu iliyomfanya Kocha Mkuu wa timu ya Wanawake ya Manchester United, Casey Stoney kuomba kubwaga manyanga.

Kocha huyo ambaye alianza kufanya kazi ndani ya kikosi hicho tangu mwaka 2018 amekuwa hana furaha juu ya vifaa ambavyo wanafanyia kazi wakati wa mazoezi tofauti na wapinzani wao Manchester City.

Casey mwenye miaka 39 amekuwa akifanya mazoezi na wachezaji wake katika viwanja vya mazoezi vya Carrington aliwashtua wachezaji pamoja na uongozi kwa taarifa hiyo aliyoitoa baada ya kuomba kuachia ngazi.

Mvutano wa ubora wa vifaa vya kutendea kazi vimefanya washindwe kuwa na maelewano makubwa na na viongozi kwa kuwa imeelezwa kuwa awali alitaka kubwaga manyanga wiki iliyopita ila uongozi ulizuia jambo hilo kwa kuzungumza naye.

Bado United hawajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo ila tayari kocha huyo amewasilisha barua ya kuomba kujiondoa katika timu hiyo pale msimu utakapomeguka.

Kwa sasa kikosi cha Manchester United kimehamia kwenye viwanja vya Carrington wakitokea Leigh Sports Village jambo lililokuwa likisababisha majeruhi kuongezeka kwenye timu hiyo kutokana na kile ambacho mwalimu amekuwa akieleza ni ubovu wa miundombinu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic